Header Ads

Header ADS

Serikali kuongeza nguvu katika kukabiliana na Wanyama Pori

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akizungumza Jijini Arusha wakati wa kikao cha nne cha Kamati  ya Usimamizi  wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya nyara ambapo amesema Wizara imejizatiti kupunguza migongano kati ya binadamu na wanyamaporiMkurugenzi wa Idara ya wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha  akizungumza Jijini Arusha wakati wa kikao cha nne cha Kamati  ya Usimamizi  wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya nyara ambapo amesema Wizara imetaendelea kutoa elimu ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifuKatibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akivishwa nembo ya UNDP na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha nne cha Kamati  ya Usimamizi  wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya nyara , Christine Musisi mara baada ya kikao hicho .

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha nne cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya nyara , Christine Musisi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wakati wa kikao cha nne cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi huo.

Serikali imesema kuwa itaendelea kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu ili wananchi wanaoishi pembezoni mwa maeneo ya Hifadhi wanufaike na maeneo hayo kwa kuendesha shughuli za utalii badala ya kulima mazao yanayopendwa na wanyamapori hao.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Arusha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka wakati wa kikao cha nne cha Kamati Tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya nyara.

Prof. Sedoyeka amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imejidhatiti katika kuhakikisha kuwa migongano kati ya binadamu na wanyamapori inathibitiwa kabla ya kuleta madhara ili wananchi waweze kufurahia uwepo wa wanyamapori. 

” Tunataka kuona migongano baina ya binadamu na wanyamapori inapungua ili wananchi wazidi kutoa ushirikiano katika kuimarisha ulinzi wa wanyamapori wakubwa wakiwemo tembo na faru ambao wapo hatarini kutoweka” Amesema Prof. Sedoyeka

Amesema wananchi wakinufaika na shughuli za uhifadhi watakuwa mstari wa mbele katika kuwafichua majangili kabla hawajawadhuru wanyamapori, hivyo Wizara inafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha wanyamapori wakali na waharibifu hawaathiri maisha ya wananchi.

  Prof.Sedoyeka amesisitiza kuwa Wizara imejipanga kutoa mafunzo kwa wanavijiji, kununua vitendea kazi yakiwemo magari pamoja na kujenga vituo vya askari kwa ajili ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu pindi wanapokaribia makazi ya wananchi.

Katika hatua nyingine , Prof.Sedoyeka ametoa onyo kwa wananchi waache kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kulima katika mapito ya wanyamapori ili kuepuka kupata hasara.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha nne cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Bashara haramu ya nyara , Christine Musisi amesema suala la kupunguza migongano kati ya Binadamu na Wanyamapori linahitaji ushirikiano baina ya Serikali na wananchi wanaoishi katika maeneo karibu na Hifadhi

” Mojawapo ya kipaumbele katika mradi wetu ni kuhakikisha tunatoa mafunzo kwa jamii jinsi ya kujikwamua kiuchumi ikiwemo ufugaji a nyuki pamoja na kutoa mafunzo wanakijiji namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu” Amesema Musisi.

Katika hatu nyingine, Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Christine Musisi amesema mradi huo utaendelea kuzinufaisha jamii kufanya shunguli zingine za kiuchumi na kuachana na vitendo vya ujangili kwa kutoa mafunzo mbalimbali ya kuwakwamua kutoka kwenye umaskini

No comments

Powered by Blogger.