Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali iliyohusisha magari matatu iliyotokea katika eneo lenye mteremko wa Iwambi na kusababisha vifo vya watoto wawili wa familia moja.

Kamanda Kuzaga amesema, chanzo cha ajali hiyo iliyotokea hii leo Novemba 9, 2022 ni mwendo kasi wa gari aina ya fuso, huku mashuhuda wakisema tukio hilo limetokea majira ya asubuhi

Inasemekana  kuwa, Dereva wa basi dogo la Abiria aina Costa katika jitihada za kulimudu gari lake alishindwa baada ya kugongana ubavuni na gari hilo dogo.

Kufuatia ajali hiyo, Kamanda Kazuga amewaomba madereva kuwa waangalifu wakati wakiendesha vyombo vya moto, ili kuepusha ajali na kuzingatia sheria za usalama barabarani.