Siku saba [7] Zatolewa kwa kamati ya ulinzi na usalama Mwanza kuwakamata waliohusika na mauaji ya Joseph Mathias
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima ametoa siku saba kwa viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo kufanya opereshi na kuwakamata waliohusika na mauaji ya Joseph Mathias mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa Kijiji cha Ngulla Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ambae ni mlemavu wa ngozi
Joseph ameuwawa kwa kukatwa panga na watu wasiojulikana kwenye mkono wake wa kulia usiku wa kuamkia Novemba 3/2022 akiwa nyumbani kwakwe.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Mwanza Alfred Kapole amesikitishwa na tukio hilo na kuiomba jamiii kuacha kufanya vitendo vya kikatili
kwa upande wake Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Mairi Makori amesema hadi Sasa tayari wanawashikilia watu watatu katika tukio hilo.
No comments
Post a Comment