Afungwa kifungo cha maisha Jera kwa kosa la kulawiti hadharani
Mahakama ya wilaya ya Tabora imemuhukumu mkazi wa Kidatu “B” kata ya Mtendeni Mkoani Tabora Husseni Mashibu (32) kifungo cha maIsha jela baada ya kupatikana na hati ya kumlawiti Mtu Mzima Hadharani huku watu Wakishuhudia kwa kumtuhumu kuwa ana Mahusiano na Mke wake .
Akitoa hukumu hiyo leo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya wilaya ya Tabora Sigwa Mzige mahakama imeona kifungo hicho kwa mshitakiwa kimstahili kwani alifanya unyama usiweze kuvumiliwa na jamii.
Alisema kifungo hicho kitakuwa fundisho kwa mshitakiwa huyo na wengine wenye nia ya kuwadhalilisha watu wengine kutokana na wivu wa mapenzi
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya Tabora Sigwa Mzige alìiambia Mahakama hiyo ushahidi uliotolewa ulitolewa mbele ya Mahakamani hiyo umeonyesha hauna shaka yoyote ukilinganisha na ushaidia uliotolewa na Mtuhumiwa Mwenyewe ,Daktari ambae alithibitisha kutokana na Vipimo vya aliye lawitiwa alipata Michubuko na alipewa dawa ya Misuli .
“Mahakama zote Nchini zinafanyakazi vizuri kuhakikisha kila Mtuhumiwa analetwa hapa kwa Makosa mbalimbali kila kosa moja lina adhabu yake”Mzige alisema
Awali Wakili wa Serikali Robert Kumwembe aliiambia Mahakama hiyo kwamba Mshitakiwa ni Mkosaji wa Mara ya kwanza anapaswa kupata adhabu ya hiyo ya kwenda jela Maisha .
Wakili huyo aliambia mahakama hiyo kwamba Mtuhumiwa alipatikana na kosa la kumlawiti mtu Mzima ( Jina limehifadhiwa ) mnamo 30 January 2022 katika maeneo ya Kidatu “B.Mkoani Tabora.
Alisema kwamba Mtuhumiwa alishitakiwa kwa Makosa Mawili ya kulawiti na kujeruhi kwa kumpiga na kitu kichwani na kumsababishia jeraha, na Makosa yote yanakwenda pamoja ikiwemo kulipa faini ya shilingi Milioni 1 .
Mtuhumiwa huyo katika Utetezi wake aliiambia Mahakama hiyo kuwa alipata tetesi kwamba Mtu huyo anamahusiano na Mke wake na siku hiyo alimfumania akiwa na mke wake ndani .
Mtuhumiwa huyo aliiomba Mahakama hiyo kuwa impunguzie adhabu hiyo kutokana na kuwa na Familia ya watu 6 na mke wake kulazwa hospitali ya rufaa Kitete kwa ajili ya kujifungua.
Mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi la Mtuhumiwa huyo kwa kuwa hukumu yake ilikuwa sawa na kosa la kumlawiti na adhabu yake ni kifungo cha Maisha jela.
No comments
Post a Comment