Serikali yawatahadharsha watumishi wa Umma wanaokiuka taratibu na kanuni za kiutumishi
Serikali imewatahadharisha watumishi wa umma wanaokiuka taratibu na kanuni za kiutumishi kwa kutoa lugha chafu kwa wananchi huku akiahidi kuwashughulikia.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere akizungumza na walimu kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Angellah Kairuki katika kikao kazi cha cha uboreshaji wa usimamizi wa elimu msingi na sekondari, kilichowakutanisha maafisa elimu Wilaya na Kata, wakuu wa shule za sekondari, na walimu wakuu wa shule za msingi mkoani hapa.
Alisema wapo baadhi ya watumishi wanaotoa lugha chafu ambazo zinarekodiwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, na kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan haiwezi kumvumilia mtumishi wa aina hiyo.
Nyerere pia amewataka viongozi hao kuwahamasisha wazazi kuthamini kwa vitendo kazi za walimu pamoja na kushirikiana vizuri na walimu katika suala la malezi na maendeleo ya taaluma ya watoto wawapo nyumbani na shuleni.
Aidha, amewataka wahakikishe wanafunzi wanapata umahiri wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu wamalizapo darasa la kwanza, na kwamba ufundishaji wa somo la kiingereza unaimarishwa kwa shule za msingi na Sekondari.
Amewataka viongozi wa elimu ngazi ya shule, kata, halmashauri na mikoa kuhakikisha wanafuatilia ufundishaji wa walimu darasani pamoja na kutatua kero za walimu kwenye maeneo yao ya kazi badala ya kukaa maofisini.
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Charles Enock Msonde kuwa amesema ili watoto wabaki salama lazima kila mmoja awe mlinzi wa mtoto na kuona kuwa ni mtoto wake.
Akitoa salamu za Mkoa Mkuu wa Mkoa katibu tawala mkoa wa wa Manyara Caroline Mthapula alisema kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Mkoa wa Manyara ulipokea kiasi cha Tsh. 3,760,000,000.00 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya 8 za Kata kupitia mradi wa (SEQUIP).
Shule 7 kati ya shule 8 zimesajiliwa na zimepokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2023.
Aidha, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Mkoa wa Manyara ulipokea kiasi cha Tshs. 1,540,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 77 vya shule za sekondari.
Hadi sasa Mkoa umekamilisha ujenzi wa vyumba vyote 77 vya madarasa sawa na asilimia 100.
Mthapula alisema hadi kufikia tarehe 10 Januari, 2023, Mkoa umeandikisha wanafunzi wa Elimu ya Awali 29,864 ambapo wavulana ni 15,564 wasichana 14,300.
Uandikishaji huu ni sawa na asilimia 64 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 46,494. Aidha, Mkoa umeandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza 44,125 ambapo wavulana 22,917 na wasichana 21,188.
Uandikishaji huu ni sawa na asilimia 77 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 57,176. Kwa kidato cha kwanza wanafunzi walioripoti ni 5,883 kwa wiki ya kwanza ni asilimia 20 ya wanafunzi 29,415 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023.
Aidha, Mkoa una jumla ya wanafunzi 1,017 wenye mahitaji maalum wakiwemo wavulana 580 na wasichana 437
Alisema Mkoa wa Manyara Mkoa una mahitaji ya vyumba vya madarasa 8,909 kwa Shule za Msingi na Awali, vilivyopo ni 5,230 na upungufu 3,679.
Mahitaji ya nyumba za walimu 6,939, zilizopo ni 2,187 na upungufu wa nyumba 4,752, Mahitaji ya matundu ya vyoo ni 16,871 yaliyopo ni 10,473 na upungufu 6,398, Mkoa unamahitaji ya madawati 134,679, yaliyopo 109,741 na upungufu 24,938.
Kwa upande wa shule za sekondari Mkoa una vyumba vya madarasa 2,153 ikilinganishwa na mahitaji halisi ya madarasa 1,919 (ziada 219).
Nyumba za walimu zilizopo ni 609 ikilinganishwa na mahitaji ya nyumba 2,990 upungufu ni nyumba 2,381.
Matundu ya vyoo yaliyopo ni 2,495 ikiwa mahitaji ya matundu ni 3,317 na upungufu
No comments
Post a Comment