Tundulissu kurudi Tanzania 25/01/2023
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema jambo kubwa atakaliliofanya atakapowasili nchini Tanzania ni kuhakikisha anaendeleza harakati za kusaka katiba mpya.
Lissu amesema hayo leo wakati akitoa salamu za mwaka mpya kwa wanachama wa chama hicho kwa njia ya mtandao ambapo amesema kama serikali na chama tawala wametangaza kuwa wapo tayari kwa mchakati huo basi CHADEMA wapo tayari kuendeleza mchakato huo.
“Rais Samia na Chama chake na Serikali yake wameshaahidi hadharani kwamba wako tayari kuanza safari hiyo ndefu na ngumu, tunawajibika kumjibu Mheshimiwa Rais kwa kuonesha na kudhihirisha kwa vitendo, kwamba na sisi pia tuko tayari na tumejiandaa kwa safari hiyo”
“Mimi binafsi na Chama chetu tuko tayari na tumejiandaa kwa safari hiyo, kwahiyo ninarudi nyumbani kwa ajili ya safari hiyo, ninarudi kwa ajili ya kazi kubwa iliyoko mbele yetu, kazi ya Katiba Mpya na mwanzo mpya kwa Taifa letu, ninafahamu licha ya ahadi ya Mheshimiwa Rais na licha ya utayari wangu na wetu, siku zijazo hazitakuwa rahisi, ninajua kuwa tutakabiliwa na majaribu ya kila aina na tutapitishwa katika tanuru kubwa la matatizo na magumu mengi." amesema Lissu.
Kiongozi huyo pia ametangaza kuwa tareje 25 Januari 2023 saa saba mchana atawasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuendeleza harakati zake za kisiasa.
No comments
Post a Comment