Header Ads

Header ADS

Watu 29 wauawa wakati wa kumkamata mtoto wa El Chapo.

 



Takriban watu 29 wameuawa wakati wa operesheni ya umwagaji damu ya kumkamata mtoto wa mfalme wa Mexico "El Chapo", mamlaka ya Mexico ilisema.

Ovidio Guzmán-López, 32, anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la zamani la babake,linalojishughulisha na dawa za kukevya alikamatwa huko Culiacán na kusafirishwa hadi Mexico City siku ya Alhamisi.

Lakini wakati na baada ya kukamatwa kwake, askari 10 na washukiwa 19 waliuawa.

Wanachama wa genge lake wenye hasira waliweka vizuizi barabarani, wakachoma moto makumi ya magari na kushambulia ndege katika uwanja wa ndege wa eneo hilo.

Wanajeshi wengine 35 walijeruhiwa na watu 21 wenye silaha walikamatwa, Waziri wa Ulinzi Luis Cresencio Sandoval alisema Ijumaa.

Bw Guzmán-López - anayeitwajina la utani "Panya" - alipakizwa kwenye helikopta na kusafirishwa hadi mji mkuu kabla ya kupelekwa katika gereza la shirikisho lenye ulinzi mkali.

Anatumiwa kwa kuongoza kundi la baba yake maarufu la Sinaloa – mojawapo ya magenge makubwa zaidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya duniani.

Baba yake, Joaquín "El Chapo" Guzmán, anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Marekani baada ya kupatikana na hatia mwaka wa 2019 ya ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

No comments

Powered by Blogger.