Ndege ya kivita ya Marekani yatungua kitu kisichojulikana
Rais wa Marekani Joe Biden aliamuru ndege ya kivita itungue "kitu cha angani" kisichojulikana kutoka Alaska siku ya Ijumaa, Ikulu ya White House inasema.
Msemaji John Kirby alisema kitu kisichokuwa na rubani ni "chenye ukubwa wa gari dogo" na kilikuwa "tishio " kwa usafiri wa anga wa raia.
Madhumuni ya kitu hicho na asili yake haikuwa wazi, Bw Kirby alisema.
Inajiri wiki moja baada ya jeshi la Marekani kuharibu puto la Uchina juu ya maji ya anga ya bMarekani.
Akiongea katika Ikulu ya White House siku ya Ijumaa, Bw Kirby alisema kitu hicho kilichodunguliwa siku ya Ijumaa kilikuwa na uchafu mdogo ikilinagnishwa na puto iliyorushwa Jumamosi iliyopita kwenye pwani ya Carolina Kusini.
Alisema kuwa kitu hicho kilikuwa futi 40,000 (12,000m)angani juu ya pwani ya kaskazini ya Alaska.
Kilikuwa tayari kimevuka Alaska kwa kasi ya (64km/h) na kilikuwa kando ya bahari kikisafiri kuelekea Ncha ya Kaskazini, ilipotunguliwa.
Mashirika ya ndege ya kibiashara yanaweza kupaa hadi futi 45,000.
Helikopta na ndege za usafiri zimetumwa kukusanya uchafu kutoka kwa maji yaliyoganda ya Bahari ya Beaufort.
"Hatujui ni kitu cha nani, iwe ya serikali au ya kampuni au cha kibinafsi," Bw Kirby alisema.
Kitu hicho kilionekana kwa mara ya kwanza Alhamisi usiku, ingawa maafisa hawakutaja wakati.
Alisema ndege mbili za kivita zilikaribia kifaa hicho na kukadiria kuwa hakukuwa na mtu ndani yake, na habari hiiiliwasilishwa kwa rais Joe Biden alkiyechaukua uamuzi huo.
"Tutaendelea kuwa macho kuhusu anga yetu," Bw Kirby alidai. "Rais anachukua majukumu yake ya kulinda usalama wa taifa letu kama jambo kuu."
Kulingana na ABC News, kitu hicho kilionekana kutokuwa na msukumo.
kilionekana kuelea, alisema mwandishi mkuu wa masuala ya kimataifa wa mtandao huo Martha Raddatz, akimnukuu afisa wa Marekani ambaye hakutajwa jina.
Katibu wa waandishi wa habari wa Pentagon Brigedia Jenerali Pat Ryder alisema kitu hicho "hakifanani kwa ukubwa au umbo" na puto ya Uchina ya wiki iliyopita.
Alithibitisha kuwa ndege ya F-22 ilidungua kitu hicho kwa kombora saa 13:45 EST (18:45 GMT) siku ya Ijumaa.
Ndege hiyo ya kivita ilitoka katika kambi ya kijeshi ya Elmendorf-Richardson huko Anchorage.
Jenerali Ryder alisema kiasi kikubwa cha uchafu kimepatikana hadi sasa. Ilikuwa ikipakiwa kwenye meli na kupelekwa kwa "maabara kwa uchambuzi ", aliongeza.
Maafisa walisema bado hawajaamua ikiwa kifaa hicho kilihusika katika upelelezi, na Bw Kirby akamsahihisha ripota aliyeitaja kama puto.
Hakutaja ni wapi hasa kitu hicho kilitunguliwa, lakini Utawala wa Usafiri wa Anga wa Shirikisho ulisema ulikuwa umefunga takriban maili 10 za mraba za anga ya Marekani juu ya Deadhorse, kaskazini mwa Alaska, kabla ya kuiagiza ndege ya F-22 .
No comments
Post a Comment