Header Ads

Header ADS

Ahukumiwa kwenda Jera kwa miaka 180 Njombe

 Mahakama ya wilaya ya Njombe imemhukumu Juma Msemwa kijana wa miaka 27 mkazi wa mkoani Njombe kutumikia jela kifungo cha miaka 30 kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika kwenye makosa sita ya ulawiti na ubakaji huku pia akitakiwa kulipa fidia ya fedha kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila muathirika kwa makosa aliyoyafanya.


Akisoma hukumu hiyo ya shauri namba 53 la mwaka 2023,Hakimu mkazi wa wilaya ya Njombe Matilda Kayombo,amesema mshtakiwa amekutwa na hatia katika makosa sita,matatu yakiwa ni ubakaji na matatu ya ulawiti anayodaiwa kuyafanya siku ya tarehe 16 hadi 23 mwezi mei mwaka 2023 katika mtaa wa kihesa kilimani mjini Njombe baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na mashahidi sabaa,wakiwemo waathirika wa matukio,Taarifa ya uchunguzi wa Daktari, uongozi wa serikali ya mtaa pamoja na Polisi.

Juma Msemwa anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti, baada ya kuwahadaa wanawake watatu na kisha kuwafungia katika nyumba aliyokuwa anaishi katika mtaa wa kihesa,na kisha kuwalawiti na kuwabaka kwa zamu usiku na mchana,zoezi lililoenda sambamba na kuwaingiza vigunzi vya mahindi na matango katika sehemu za siri.

Taarifa zilizosaidia kukamatwa kwake zinaelezwa na Mahakama kuwa zilitolewa na mmoja kati ya wanawake aliokuwa amewateka,ambae alifanikiwa kutoroka na kupiga ndulu kwa majirani ambao walivamia nyumbani kwa Juma na kukuta wanawake wengine wawili wakiwa ndani,vile vile kulikutwa mfuko ukiwa na dawa za kienyeji huku Mahakama ikieleza kuwa sehemu ya ushahidi uliotolewa ulibainisha kuwa mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kwamba alifanya matukio hayo akiwa anatekeleza maagizo ya mganga aliyemtaka abake wanawake na watoto.
Waendesha mashtaka wakiongozwa na Magdalena Whelo na Elise James waliiomba mahakama kutoa hukumu kali kwa mtuhumiwa ili iwe funzo kwa jamii ikizingatiwa matukio ya ubakajai na ulawiti yamekuwa yakiongezeka maradufu Njombe ambapo baada ya Mahakama kujiridhisha na ushahidi imemhukumu Msemwa kutumikia miaka 30 jela kwa kila kosa,katika makosa yote sita aliyokutwa nayo,ambayo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili (e) sambamba na kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya adhabu kifungu namba 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.


No comments

Powered by Blogger.