Wanafunzi watakiwa kuachana na matumizi ya Simu za Mkononi
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bweni ya Wavulana Oswe wametakiwa kuachana na matumizi ya simu za mkononi ikiwa ni pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuepukana na wimbi la mmomonyoko wa maadili katika makuzi yao na kupelekea kupoteza malengo kwenye masomo yao.
Akizungumza na wanafunzi hao Oktoba 17, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya, alisema kwa sasa jamii imekumbwa na changamoto nyingi hasa kwenye suala la malezi ambalo limepelekea watoto wengi kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa.
Aidha, kamanda Mallya aliendelea kuwasihi wanafunzi hao kuchagua aina ya marafiki ambao watakuwa kimbilio kwao na msaada katika makuzi yao.
No comments
Post a Comment