Header Ads

Header ADS

Timu ya Bayern Munich itakalibiana na ushindani wa klabu mbili ligi kuu uingereza

 


.

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Joao Palhinha

Timu ya Bayern Munich itakabiliana na ushindani kutoka kwa klabu mbili za Ligi Kuu ya Uingereza wakati wa kumnunua kiungo wa Fulham na Ureno, Joao Palhinha (28), mwezi Januari - limeandika gazeti la Telegraph.

Bayern wanaweza kumkosa kiungo wa kati wa Bayefdcer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Florian Wirtz pia, kwani Manchester City na Liverpool zina nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, mtandao wa 90min unaeleza.

Mshambulizi wa Gremio na Uruguay, Luis Suarez (36), anatazamiwa kuungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami kwa mkataba wa mwaka mmoja. (Miami Herald)

rtfgv

CHANZO CHA PICHA

Maelezo ya picha,

Julen Lopetegui

Kocha wa zamani wa Wolves, Julen Lopetegui alikataa kandarasi ya pauni milioni 15.4 za Uingereza kwa msimu kutoka kwa timu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia akitaka kusalia kwenye Ligi ya Kuu ya Uingereza, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyohusishwa kutaka kumwajiri Mhispania huyo. (AS)

Kitahitajika kitita cha pauni milioni 60 kwa Aston Villa kufikiria kumuuza Douglas Luiz ifikapo mwezi Januari, huku Arsenal ikionyesha nia ya kutaka kumnunua kiungo huyo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 25. (Caught Offside)

Arsenal na Liverpool zote zilituma mawakala kumtazama beki wa pembeni wa Bayer Leverkusen na Uholanzi, Jeremie Frimpong (22). (90min)

Real Sociedad wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza, Mason Greenwood (22), ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Getafe. (Todofichajes)

rgfv

CHANZO CHA PI

Maelezo ya picha,

Van de Beek

Donny van de Beek wa Manchester United amejitoa kwa Barcelona, kiungo huyo wa kati wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 26 - anatumai ataziba pengo la kuumia Gavi. (Sport)

Wakati huo huo, Manchester United inatazamiwa kumsajili winga wa Borussia Dortmund na Uholanzi, Donyell Malen (24), ikiwa winga wa Uingereza, Jadon Sancho (23), ataondoka katika klabu hiyo. (Football Transfers)

Wolves wanavutiwa na beki wa pembeni wa Sevilla na Argentina, Marcos Acuna (32), anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni za Uingereza milioni 10.3. (Todofichajes)

Timu ya Sao Paolo wako tayari kumuuza mchezaji anayelengwa na Liverpool, Lucas Beraldo, wakati Wolves ilikataliwa ombi la kumnunua mlinzi huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 20 msimu wa joto. (90min)

Juventus wako tayari kumwachia winga wa Uingereza, Samuel Iling-Junior kuondoka mwezi Januari huku Tottenham na Newcastle wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Tuttomercatoweb)

West Ham, Everton, Brighton na vilabu vingine vya Ligi Kuu ya Uingereza viko katika kinyang'anyiro cha kumnunua mshambuliaji wa Linfield mwenye umri wa miaka 17 na Ireland Kaskazini, Aodhan Doherty. (Football Insider)


No comments

Powered by Blogger.