Header Ads

Header ADS

Walioguswa na maafuriko ya Hanang Mkoani Manyara waendelea kuchangia misaada

 


Na Biesha Ibrahim-Manyara

 Mhe. Jenista Mhagama ambaye ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu Bunge na uratibu ameelekeza watendaji wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika ofisi hiyo kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kimfumo ili misaada yote iingie kwenye mfumo rasmi ili iweze kuwafikia wale waliokusudiwa.

Ameyasema hayo wakati akipokea vifaa vya msaada wa kibinadamu vilivyowasilishwa na wadau mbalimbali kusaidia wahanga wa maafa yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang Mkoani Manyara.

Waziri Mhagama alisema Serikali imepokea misaada hiyo huku akishukuru kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwahakikisha kuwa misaada hiyo itasimamiwa kwa ukaribu ili kuhakikisha inaleta tija kwa wahusika.

“kipekee niwapongeze na kuwashukuru sana kwa namna mlivyoguswa na kuungana na Serikali katika kuwanusuru ndugu zetu waliopatwa na maafa haya, Hanang Tunawashukuru sana,” alisisitiza

Pia ametoa angalizo kwa yeyote atayejaribu kufanya wizi au utapeli katika kipindi hiki
“Tumewaonya matapeli wasije wakathubutu kutengeneza akaunti za utapeli kwa sababu tutawakamata na serikali itachukua hatua kali za kisheria,” alibainisha

Aidha Waziri amesema serikali imetoa akaunti namba ili kusaidia kukusanywa kwa michango hiyo
“Kwa ajili ya kukabiliana na maafa ya Katesh itatumika  Akounti ya Mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (National Disaster Management Fund Electronic Account) Na. 9921151001 kwa kuandika neno maafa likifuatiwa jina la Wilaya ya Hjanang’.

Halikadhalika alitoa rai kwa watumishi watakaohusika na misaada itakayotolewa kuhakikisha wanafanya kazi kwa uaminifu ili misaada iwafikie walengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe.Mary Chatanda alisema anatoa pole kwa niaba ya Umoja wa wanawake Tanzania kwa tukio hilo lenye kuleta majonzi na huzuni kubwa kwa wana Hanang’,  jamii na Taifa kwa ujumla.

Tunashukuru wafadhili mbalimbali wameweza kutuchangia, tumekuja na Mablanketi 120, mashuka 300, mashuka ya kimasai 500, madira ya kuvaa wanawake 520, kanga 1000, katoni za sabuni na mafuta ya kupaka,” alisema

Aidha alitoa rai kwa jamii, wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia ili kuwapa nafuu waliofikwa na maafa hayo.

“Wabunge wetu wa viti maalum nao wamesaidia kuchangia kupitia kwa Ktibu wao wa wabunge na fedha hizo tutawasilisha baadae,” alieleza Mhe. Chatanda.






No comments

Powered by Blogger.