Wananchi wakiwa kwenye foreni ya maji katika mji wa Makambako
Wananchi wa Mji wa Makambako Mkoani Njombe wakiwa kwenye foreni ya maji .Tatizo la maji katka mji wa Makambako limesababisha kudorora kwa shughuli mbalimbali za uchumi.Akizungumza Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema mheshimiwa Oraph Muhema ,Amesema iwapo atapita kuwawakilisha wananchi Bungeni atahakikisha kipaumbele chake cha kwanza ni kutatua kero ya maji katika Mji wa Makambako.
Mmoja kati ya wananchi amesema wanalazimika kutoka saa tisa usiku ili kuwahi foreni ya maji hali inayosababisha kukwamisha maendeleo na uchumi wa wakazi wa Makambako,Piahali hii inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kwani maji yanayo tumiwa na wananchi wa Makambako ni machafu kabisa.Kwaupande mwingine wananchi wameitaka Wizara husika kuingilia kati kutatua tatizo hilo la maji.
No comments
Post a Comment