Header Ads

Header ADS

Operesheni maalumu katika msitu wa hifadhi YA Biharamlo yabaini ma`shamba makubwa ya bangi



















 Kikosi kazi cha kudhibiti usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya kinacho husisha jeshi la wananhi,Mgombo,Magereza,Uhamiaji na polis wa wilaya ya Biharamulo Mkoa wa kagera kimeanzisha operesheni maalumu ktk msitu wa hifadhi ya Biharamulo na kubaini uharibifu mkubwa wa mazingira Ikiwemo ukataji miti ya upasuaji mbao,uchomaji mkaa,ufugaji,Kilimo cha mazao ya chakula na dawa za kulevya aina ya bangi kinyume cha sheria za nchi.
             Hao ni baadhi ya askili wa kikosi kazi cha kudhibiti dawa za kulevya wakifurahia baada ya kukamata watuhumiwa na kuteketeza shamba la dawa za kulevya aina ya bangi lenye ukubwa wa hekali kumi{10}ktk msitu wa hifadhi ya biharamulo eneo la nyatakara na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye amekili kuhusika na kilimo chambangi na kusema kwamba amelazimika kulima zao la bangi kwa lengo la kupata fedha kuwasomesha wadogo zake.
              Kwa upande wa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Biharamulo anaye ongoza kikisi kazi cha kudhibiti dawa za kulevya wilani humo Bi.saada mulunde amesema kwamba oparesheni hiyo endelevu ktk misitu ya hifadhi itakapo kamilika itaendelea Nyumba kwa nyumbakwa` lengo la kuwakamata wafanya biashara,wasambazaji wa dawa za kulevya baadhi y wananhi wameiomba serikali kutoa elimu kwa jamii mjini,vijijini jinsi ya kukabiliana na dawa za kulevya ambaza zinapoteza ngu kazi ya taifa.

No comments

Powered by Blogger.