Header Ads

Header ADS

Taarifa ya uchunguzi wa kifo cha Farujohn aliyoipokea waziri mkuu

     Kama unakumbuka December 10,2016 waziri mkuu Kassim Majaliwa aliunda tume baada ya kupokea pembe mbili za Farujohn na taarifa zenye nyaraka zilizotumika kumhamisha faru huyo.Hatua hiyo ilifuatia agizo alilolitoa December 6,2017 akiwa ziarani mkoani Arusha ,ambapo alitoa siku mbili na kuutaka uongozi wa mamlaka ya hifadhi Ngorongoro[NCAA],umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha Farujohn kutoka kwenye hifadhi hiyo.








       Machi 27,2017 Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa rasmi ya uchunguzi wa kifo cha  Farujohn kutoka kwa mkemia mkuu wa serikali Prof,Samwel Manyele ambaye alikuwa akiongoza tume maalum iliyoundwa na waziri mkuu.
       Akisoma taarifa hiyo mbele ya waziri mkuu Prof. manyele amesema tume yake ilifanya uchunguzi wa kifo cha Farujohn kwa kupima vinasaba ya sampuli mbalimbali vikiwemo Mzoga,Fuvu,Mifupa,Pembe,Damu,Ngozi na kinyesi kilichokaushwa ambapo ilibainika kuwa vyote ni vya mnyama mmoja aina faru mweusi ambaye ni dume.
      Prof.Manyele amesema matokeo hayo yamethibitisha kuwa farujohn alikufa katika hifadhi ya Sasakwa Grumeti kwa kukosa matunzo na uangalizi wa karibu.
     Maabara iliyotumika ni ya chuo kikuu cha Pretoria Afrika kusini chini ya usimamizi wa timu ya wataalamu kutoka tanzania,wachunguzi wa serikali, chini ya ofisi ya mkemia mkuu wa serikali.Sababu za kifo chake zilichangiwa na kukosa matunzo na uangalizi wa karibu kukosa matibabu alipoumwa,mazoea yanayotokana na kutofuata taratibu zilizowekwa kisheria na mapungufu ya kiuongozi kwa wizara husika  hifadhi na taasisi zake.
    Prof.Manyele amesema mapungufu waliyoyabaini kutokana na uchunguzi huo ni kutokuwa na kibali rasmi cha kumhamisha farujohn,kukosekana kwa mkataba wa kupokelewa kwa farujohn hifadhi ya Sasakwa Grumeti na kutofuatiliwa kwa afya a maendeleo ya farujohn baada ya kuhamishwa.
    Mengine ni uchukuaji holela wa sampuli za wanyamapori kwa lengo la utafiti na kuzisafirisha nje ya nchi.Migongano ya kimaslahi kati ya watumishi waliolenga kusimamia taratibu za wale wenye kusimamia maslahi yao binafsi na uwepo wa taasisi nyingi zenye mamlaka sawa juu ya hifadhi ya wanyama pori  ''Pamoja na kwamba mawasiliano yanaonyesha zoezi hilo liliridhiwa na wizara hapakuwepo na kibali rasmi kutoka kwa mkurugenzi wa wanyama pori cha kuruhusu kumhamisha farujohn kutoka NCAA Kwenda Grumeti Prof.Manyele katika ripoti yake''
     Akizungumza kuhusu uchukuaji holela wa sampuli za wanyamapori kwa lengo la utafiti na kuzisafirisha nje ya nchi .
    Prof.Manyele amesema kumbukumbu za utafiti na aina ya sampuli wanazochukua haziwekwi vizuri na kwamba tume inashauri TAWIRI na TANAPA wapewe msisitizo juu ya umuhimu wa kuzingatia majukumu yao.
      Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusomewa ripoti hiyo waziri mkuu alishukuru timu ya uchunguzi iliyokuwa chini ya mkemia mkuu wa serikali kwa kazia aliyoifanya ikiwemo kuainisha udhaifu uliokuwemo ndani ya wizara ya maliasili na utalii na taasisi zake
    Ofisi yangu itaipitia taarifa hii ambayo ni kubwa kiasi cha kuifanyia kazi,tutayatoa hivi karibuni ili kuonyesha serikali imeamua kufanya nini juu ya mapendekezo yaliyotolewa.

1 comment

MACHWEO MEDIA said...

weka koment yako na siyo matusi

Powered by Blogger.