Header Ads

Header ADS

Ratiba ya mkutano wa saba wa bunge linaloanza leo Jumanne April 4.


























Waziri wa fedha na uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi  Juni 15 mwaka huu.
      Tarehe hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya mkutano wa wa saba wa bunge linaloanza leo jumanne[April 4]katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma ,Mkutano huo ni maalum ya bajeti.
      Ratiba hiyo inaonesha shughuli za kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika mashariki siku ya jumanne na bajeti ya ofisi ya waziri mkuu itasomwa siku ya Alhamisi April 6 na kujadiliwa kwa siku nne ikifuatiwa na Bajeti ya rais [siku 4]na bajeti ya makamu wa rais siku 1,kabla ya bajeti ya wizara ya sheria na katiba April 25.
    Mbali na bajeti za wizara mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada kadhaa ya sheria ukiwemo muswada na sheria ya marekebisho ya sheri mbalimbali wa mwaka 2017.


No comments

Powered by Blogger.