Header Ads

Header ADS

SAKATA LA KUIBIWA MTOTO:Waziri Ummy aunda tume huru kuchunguza.

       Siku zimepita tangu sakata la mwanamke mkaazi wa Dar es salaam aitwae Asma kudai kuibiwa mtoto ambaye alidaiwa wakati akifanyiwa Ultra Sound alikua na ujauzito wa watoto mapacha lakini alipokwenda kujifungua aliambiwa amejifungua mtoto mmoja..
           Baada ya kuwepo kwa mkanganyiko huo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameamua kuingilia kati kuunda tume huru ya wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuchunguza na kubaini ukweli..
         "Baada ya kufuatilia hayo..Nikiwa Waziri mwenye dhamana,nikiwa na wajibu wa kutenda haki nimeamua kuunda timu huru ya kuchunguza suala hili ambyo itaongozwa na Prof.Charles Majinge daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama ambaye ndiye atakayekuwa mwenyekiti -Ummy Mwalimu..
            Bi Asma Juma mkaazi wa Mbande DSM alilalamikia uongozi wa Hospitari ya Temeke baada ya kudai kuibiwa mtoto baada ya kujifungua akisema alikuwa na ujauzito wa mapacha.Jambo ambalo lilipelekea Mganga mkuu wa mkoa Dr.Grace kuunda tume ya kuchunguza ukweli ambaporipiyi ilisemakuwa Bi Asma alikuwa na ujauzito wa mtoto mmoja lakini ripoti hiyo ilipingwa na familia.  

No comments

Powered by Blogger.