Header Ads

Header ADS

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoani Njombe Jimbo la Makambako cha zindua operation Amsha Dude.

       Kwa mjibu wa Chama hicho operation  Amsha Dude inalenga kuhakiki uhai wa Chama ,Kuleta hamaza kwa wanachama na kufanya maandalizi ya uchaguzi ndani ya Chama hicho.
     Hayo yametolewa leo julai 15,2017.na mwenyekiti wa zoezi hilo la operation Asha Dude  mheshimiwa  Diwani George  Nelsoni Sanga .ambaye ni diwani katika kata ya Ramadhani Njombe mjini wakati akizungumza na wanachama wa jimbo la makambako.




























   Naye katibu  wa operation hiyo Mheshimiwa Oraph  Mhema ambaye ndiye alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo hilo la Makambako ,alisimama na kuelezea hali ya kisiasa ya ndani ya Chama na kusema hali ya kisiasa ndani ya chama ni nzuri  na Bado Chadema tupo vizuri" Alisema  Oraph Mhema.Pia aliendelea kusema kuwa japo kuna mbinu zinazofanya na chama cha mapinduzi kuwanunua baadhi ya madiwani wa Chadema  Chama bado kipo hai na hakiteleki .
    Oraph ambaye Ndiye katibu wa Operation Amsha Dude  aliendelea kusema kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 chama kiliruhusu kugombea kila aina ya watu pasipo kujali hata kama ni mwanachama kajiunga leo na chama ndio maana sasaivi ina fika mwafaka viongozi waliopewa dhamana na wananchi kuwa watakuwa watetezi kwa wananchi wamegeuka kuwasaliti wananchi kwa kununuliwa na chama cha mapinduzi akitolea mfano  madiwani waliojihudhuru kutoka Kilimanjaro eti ni kwa sababu walizozisema wanamuunga utendaji kazi wa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kumbe wamesha nunuliwa na upande mwingine wa pili.

No comments

Powered by Blogger.