Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamini Wiliamu Mkapa amewasili wilaya ya Chato akiwa na mke wake mama Anna Mkapa .
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa ,anatarajia kukabidhi nyumba kumi [10] kesho Julai 10 2017 kwa hospitali ya Wilaya ya Chato zilizo jengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.
Katika msafara wa Benjamini Wiliamu Mkapa ,Ameambatana na Balozi wa Japani wa hapa Tanzania Masaharn Yoshida ambaye kesho juma tatu julai 10 ,2017 atakabidhi mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti kwa chama cha Ushirika wa kilomo na masoko Chato, AMCOSS.
Pia Rais Mstaafu Benjamini Mkapa anatarajia kuhudhuria mkutano wa hadhara utakao hutubiwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania . DK. John Pombe Magufuli kesho jumatatu katika Uwanja wa Mazaina Chato Mjini.
No comments
Post a Comment