Header Ads

Header ADS

Siku moja baada ya Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tamisemi za Serikali za mitaa George Simbachawene kuongea jinsi uzembe ,unyanyazaji wa wagonjwa na waliofiwa katika hosipitali ya Sinza Parestina manispaa ya ubungo . Mganga mkuu wa Hospitali hiyo ameomba asaidiwe kufichua madudu zaidi





















Dk Mariamu  Majaliwa ,Ambaye ndiye Mganga mkuu wa Hospitali hiyo  ameyasema hayo alipotakiwa kuzungumzia kilio cha  watu wengi kuhusu utendaji  kazi wa Hospitali yake, Akiwemo Waziri Simbachawene alipozungumza na mtandao huu kuwa mke alishuhudia mwili wa kaka wa Waziri huyo ukitupwa kwenye gari mithili ya mzoga,tena baada ya maneno mengi ya kejeli kwa wafiwa.
  Dk  Maliam Majaliwa amesema kwa sasa anaomba apewe muda ili aweze kufanyia kazi malalamiko yaliyotolewa na Waziri Simbachawene. Hata hivyo amesema kama kuna malalamiko mingine kutoka kwa wananchi walio hudumiwa katika hosipitali hiyo na kukutana  na shida mbalimbali wafike hospitalini ili wamuone wakiwa na maelezo kamili.
  

No comments

Powered by Blogger.