Header Ads

Header ADS

Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema DK Vicent Mashinji na wabunge wawili wakamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma.

Vicent Mashinji ,Ambaye ndiye katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Taifa alikamatwa na wabunge wawili wa chama hicho jana nakushikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Ruvuma  wakati wakiwa kwenye kikao cha ndani .
    Wabunge ambao alikuwa nao ni pamoja na Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe, Ambaye ni mwenyekiti wa Chadema kanda ya kusini pamoja na Mbunge viti maalumu Mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakaru  kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia  wanasiasa hao wanashikiliwa na jeshi la polisi katika  Wilaya ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma
    Imeelezwa kuwa polisi waliwavamia wanasiasa hao na kuwakamata wakati wakiwa kwenye kikao cha ndani kilicho kuwakinaendelea ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu  Mkuu kukagua shughuli za Chama katika majimbo ya kanda.


No comments

Powered by Blogger.