Header Ads

Header ADS

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka aangiza Halmashauri ya Wilaya ya Makete kuruhusu wananchi kufanya biashara katika maeneo yao.



















           Christopher Olesendeka, ambaye ndiye Mkuu wa Mkoa wa Njombe ameiagiza Wilaya ya Makete  kuruhusu Wananchi wa Kata ya Lupila kufanya biashara katika maeneo yao ilikuwapunguzia umbali mrefu waliokuwa wakitembea kufika katika soko la Kata hiyo hapo awali.
            Agizo hilo amelitoa leo kufuatia maombi ya wananchi hao waliodai kufungiwa maduka yao katika nyumba na kulazimishwa kufanya biashara katika soko lililojengwa na Halmashauri hiyo ambapo lipo umbali wa kilometa moja kutoka sehemu ya makazi.
            Naye Mzee Daniel  Sanga , ambaye ni mmoja kati ya wananchi amesema kuwa kutokana na maamuzi hayo ya Mkuu wa Mkoa  itawaondolea usumbufu wa kutembea umbali mrefu  pia itawavutia kufungua maduka jirani na nyumba zao.
            Daniel  Okoka , ni Diwani wa Kata ya  Lupila " amesema kijiji hicho kimekuwa na changamoto  ya matumizi ya soko kutokana na mvutano uliopo kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Makete na Wananchi  wa Kata ya Lupila.

No comments

Powered by Blogger.