Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chazungumzia hali ya uchumi nchini.
Baada ya Kamati kuu ya Chadema kukaa kwa siku mbili mfululizo july 29 na 30/ 2017 Katika Hotel ya Double Tree jijini Dare s Salaam, kujadili mambo mbalimbali na kukubaliana kuchukua hatua . Chama hicho ambacho ndio chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimeamua kukutana na waandishi wa habari july31/2017 kupitia mwenyekiti wa chama hicho mheshimiwa Freemani Mbowe na kuongelea maswala mazima ya uchumi wa nchi.
Miongoni mwa mambo waliyozungumzia baada ya kamatikuu ya CHADEMA ni maswala la uchumi ambapo mwenyekiti wa Chama hicho Freemani Mbowe alisema vipo vigezo vingi ambavyohutumika kupima uchumi,Mbowe ,amesema umhimu wa vigezo husika huwa na maana kutegemeana na namna vinavyo athiri maisha ya wananchi.
No comments
Post a Comment