Kiongozi wa Upinzani Nchini Kenya Laila Odinga amepinga matokeo yanayotangazwa na IEBC.
Laila Odinga ,ambaye ndiye Mgombea Uraisi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani Nchini Kenya National Super Alliance [NASA] .Leo asubuhi 9/8/2017 Ameibuka na kupinga matokeo ambayoyalikuwayakiendelea kutangazwa na Tume ya Uchaguzi Nchini Kenya.IEBC.
Kwa mjibu wa taarifa zilizotufikia kutoka Nchini Kenya ,kiongozi huyo wa upinzani Laila Odinga amezungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa Tume ya Uchaguzi imekuwa ikitangaza matokeo kwenye tovuti bila kufuata utaratibu unaotakiwa.
Baada ya kufungwa kwa baadhi ya vituo kufuatia kutamatika kwa zoezi la upigaji kura matokeo yalianza kutangazwa na kumuonyesha Rais Uhuru Kenyatta ,akimshinda Odinga.
Mpaka kufikia saa moja asubuhi siku ya juma tano 9/8/2017 ,Uhuru alikuwa anaongoza kwa kura milioni 9.1 na Odinga akiwa na kura milioni 5.6. Laila Odinga ambaye amewania Uraisi kwa mara ya nne, amesema kwamba matokeo yoyote yanayotangazwa bila kuwepo kwa fomu 34A kutoka Vituoni si halali.Nakusisitiza kuwa muungano wa Vyama vya Upinzani yaani NASA hautambui matokeo hayo yanayotangazwa na vyombo vya habari na kuitaka Tume itoe fomu 34A.za kila kituo kabla ya matokeo zaidi kutangazwa
Tume ya uchaguzi Nchini Kenya IEBC ,imesema hakuna dosari iliyopo na kwamba fomu hizo zitawasilishwa kwa muungano wa NASA na Vyama vingine vya kisiasa kupitia barua pepe.
No comments
Post a Comment