Header Ads

Header ADS

Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma hatarini kuwa jangwa.

Mkuu wa Wilaya ya Songea MKoani Ruvuma  Polole Mgema amesema Wilaya hiyo inakabiliwa na tishio la kugeuka jangwa kutokana na wananchi kukata miti ,kuchoma moto mistu ovyo na baadhi ya watumishi wasiyo kuwa waadilifu kuruhusu wafugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini kuingiza idadikubwa ya mifugo bila kufuata sheria.
                                                                                                                                                                                              Mkuu huyo wa Wilaya ameendelea kwa kusema kuwa kuna uhalibifu mkubwa hasa katika mlima Lihanje na amekuwa akitoa maagizo kwa watendaji wake mara kwa mara kusitisha shughuli za kilimo katika mlima huo hata hivyo kuna baadhi ya wananchi wanaonekana bado wanaendelea na kitendo cha kukata miti
          Kitendo ambacho ameamua kufanya yeye mwenyewe Mkuu huyo wa Wilaya operation ya kuwaondoa wafugaji pamoja na wakulima wanaokaidi kuondoka na kusema kwamba wasije wakalalamika kitakachojitokeza.

No comments

Powered by Blogger.