Yono Stanley ,anashikiliwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kutoa rushwa.
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa Nchini TAKUKURU Kanda ya kati inamshikilia aliyekuwa mgombea nafasi ya uwakilishi kanda Yono Stanley.Yono Stanley alikuwa anawaniakuwakilisha mikoa ya Ruvuma na Njombe anashikiliwa na TAKUKURU na kuhojiwa kwa tuhuma za kutaka kuwahonga wajumbe iliwamchague kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Ramadhani Mambosasa kuwa mgombea alikutwa na jumla ya sh 500000/=Kwenye choo ambacho kipo nje ya ukumbi wa uchaguzi.
Ramadhani ,alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amezipanga hela hizo katika mafungu ya sh 50000/=kwenye kila bahasha.
No comments
Post a Comment