Kiongozi wa Upinzani Nchini Kenya atangaza kutoshiriki katika uchaguzi mkuu wa marudio utakaofanyika tarehe 17 octoba 2017.
Raila Odinga, ambaye ndiye kiongozi mkuu wa upinzanzani nchini Kenya ametangaza kuwa hayupotayari kurudio marudio ya uchaguzi nchini humo.
Odinga ameyasema hayo wakati akitaka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika ,kabla ya yeye kukubali kushiriki katika uchaguzi.
Pia kiongozi huyo ameendelea kusema kuwa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya ibadilishwe kwa kuwa imelaumiwa na Mahakama ya juu kwa kuendesha uchaguzi kwa njia ambayo haikuwa nzuri na kusababisha kufutiliwa mbali kwa matokeo.
Ikumbukwe kuwa Tume ya Uchaguzi ilishatangaza toka 4/9/2017 siku ya marudio ya uchaguzi kuwa itakuwa tarehe 17 octoba 2017.Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chibukati amesema uchaguzi huo utahusisha wagombea wawili ambao ni Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.
No comments
Post a Comment