Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limemkamata Mchungaji Peter Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa [CHADEMA] amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa jukwani akifanya mkutano wa hadhara Jimboni kwake
Mbunge huyo amekamatwa akiwa anahutubia wananchi wa kata ya Mlandege Jimboni humo kwa mjibu wa taarifa zilizotufikia ghafla Jukwaa lilizungukwa na Asikali wa kutuliza Ghazia [FFU] na kumtaka kushuka jukwani .
Msigwa alitii na kushuka na hatimaye moja kwa moja Askali walimchukua na kumpeleka kituo cha Polisi cha Iringa Mjini.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Julius Mjengi amedhibitisha kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Iringa Mjini.na kusema taarifa zaidi ya kukamatwa kwake itatolewa baadaye.
Imechapishwa na GEORGE MWITA
No comments
Post a Comment