Joshua Nassari ,afichua siri ya Madiwani Chadema kujihudhuru Arusha
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akihutubia wananchi katika Jimbo lake ametoa sababu zinazo wafanya Madiwani wa Arusha kupitia tiketi ya CHADEMA kujihudhuru na kuzingizia kwamba wanaunga mkono utendaji wa Rais .John Magufuli .
Nassari amesema anaushahidi wa kielektroniki kuwa madiwani hao walihongwa rushwa ili wajihudhuru nafasi zao.Akizungumza na Wananchi wa Jimbo lake Nassari amesemma amekuwa akijiuliza kwa kipindi kirefu sana alipokuwa masomoni Nchini Uingereza ni kwanini Madiwani wa Arusha wanajihudhuru ndipo alipoamua kufanya uchunguzi wa kina
Nassari ,ambaye aliongozana na Mbunge wa Arusha mjini Mh: Godbless Lema katika mkutano huo amesema alianza kufanya uchunguzi huo mei kwa kutumia vifaa vya kielektroniki alivyo vinunua nchini Uingereza na kubaini kuwa baadhi ya Madiwani wanaojihudhuru walipewa rushwa ya fedha na ahadi ya vyeo.alisema kuwa hakuna Diwani aliyejiuzuru kwa kumuunga mkono Rais bali madiwani wote walojiuzuru walipewa rushwa.
No comments
Post a Comment