Rais ,wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR Jonh Pombe Magufuli ,Amesema hawezi kuongeza mishahara mipya kwa watumishi wa umma.
Raisi, Pombe Jonh Magufuli , Ameyasema hayo jana alipokuwa akifungua mkutano wa 33 wa jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania [ALAT].Ambao uliwakutanisha Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri Nchini.
Magufuli amesema tangu alipoingia madarakani hajapandisha mishahara ya watumishi wa Umma na hatapandisha kwa sababu anawatumikia Watanzania kwanza.Pia Rais, Magufuli alieleza umhimu wa ALAT katika kukamilisha majukumu wa kufuata ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi [CCM] na mikakati yake kwa Watanzania kama alipokuwa akiahidi kwenye kampeni zake za mwaka 2015 kushughulikia changamoto za uhaba wa watumishi katika Halmashauri ,na ucheleweshwaji wa ruzuku wa miradi ya maendeleo.
No comments
Post a Comment