Mtu mmoja Nchini Kenya aliyetambuliwa kwa jina la Patrick Odoyo amepoteza fahamu na kufariki wakati wa kupiga kura katika eneo la Nyando Kisumu Kenya.
Patrick Odoyo ndiye mtu aliyekuwa wa tano wakati wa upigajikura katika kituo cha Kata ya Kobura alipoteza fahamu na kukimbizwa katika kituo cha Afya cha Ahero ambako juhudi za kunusuru maisha yake zilishindikana na kupelekea kifo.Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti .
Kwa mjibu wa taarifa zilizotufikia hivi punde mpaka sasa haijajulikana chanzo cha mtu huyo kupoteza fahamu mpaka kufariki .Lakini vyanzo vya habari vinaeleza kuwa watu wengi wametoka nyumbani alfajiri kuwahi kupiga kura bila kula kitu chochote na hali mbaya ya hewa.

No comments
Post a Comment