Header Ads

Header ADS

Madiwani waliohama Chadema waangukia pua kura za maoni CCM


























         Chama cha Mapinduzi CCM,  Mkoa wa Arusha kimewateua wagombea nane wa udiwani watakao shiriki katika uchaguzi mdogo  watatu wakiwa ni Madiwani waliojiuzulu kutoka Chadema  kwa kutoa sababu ya kuwa wanamuunga mkono jitihada za Rais Jonh Magufuli.
         Lakini hali imeenda tofauti tofauti ya matarajio yao na kujikuta wanadondoshwa kwenye kura za ndani ya CCM,Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM wa Mkoa wa Arusha ,Shaabani Mdoe ,Amesema kuwa Madiwani hao walio pitishwa watapeperusha bendera ya CCM.katika uchaguzi mdogo wa Madiwani.
      Mdoe ,Amesema kuwa katika kikao hicho  wajumbe wote wamekubaliana na kutoka kwa kauli moja kuhakikisha ushindi unapatikana kwa chama cha Mapinduzi na kuzitwaa kata zote ambazo zilikuwa zikishikiliwa na Chadema.

No comments

Powered by Blogger.