Mbunge wa Arusha Mjini Lema alaani vikali tukio la kukamatwa kwa wafuasi wake.
Godbless Lema ,Amelaani vikali kitendo cha kuwakamata wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa madai yaliyotolewa na Chama cha Mapinduzi [CCM] kuwa walihusika kumpiga mgombea wao hivi karibuni.
Mbunge huyo amesema kuwa madai hayo hayana ukweili ni uongo na kufananisha kuwa ni sawa na poropoganda za siasa maji taka katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi .Kuhusiana na uchaguzi mdogo wa Madiwani Mbunge huyo wa Arusha Mjini amesema kuwa kama CCM hawatabebwa hawana uwezo wa kushinda hata kata moja.
Ameendelea kusema kuwa wasidhani kushinda ushaguzi huu kwa sababu wanavyombo vya Dola , Wananchi wataamua kupitia sanduku la kura na ninaimani hawatapigia kura za ndiyo kwa CCM 'alisema.
No comments
Post a Comment