Mfumuko wa bei 2018 iliyotolewa na NBS.
Serikali imesemakuwa Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi january 2018 umendelea kubaki palepale asilimia 4.0 kama ilivyokuwa mwezi disemba 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Da res Salaam Mkurungezi wa Takwimu za jamii Ephraimu Kwisigabo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesemakuendelea kubaki palepale kwa Mfumuko wa bei wa mwezi january 2018 kumechangiwa na bei za bidhaa za vyakula kutobadilika.
Kwa mjibu wa bwa Ephraim , amesema kuwa baadhi ya bei za vyakula zinazochangia mfumuko wa bei kubaki asilimia 4.0 kati ya mwezi january 2017 na mwezi january2017 ni pamoja na mahindi kwa asilimia 8.0 ,Maharagwe kwa asilimia 4.3, Samaki asilimia 9.0 na ndizi za kupika asilimia 9.0.
Aidha aliendelea kusema kuwa baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula zilichangia mfumuko wa bei kwa mwezi januari2018 ,kubaki palepale ni pamoja na sare za shule kwa asilimia 2.3,huduma za afya katika hospitali binafsi asilimia 10.0 mkaa asilimia 9.4, vitabu vya shule asilimia 2.7, na gharama za malazi kwa asilimia 3.2.
Pia amesema kuwa mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika mashariki kama nchi ya Uganda.
No comments
Post a Comment