Umoja wa kimataifa umeikosoa serikali ya Kenya kwa kukaidi amri ya mahakama .
Ofisi ya Kamishina wa haki za binadamu wa umoja wa kimataifa imekosoa hatua ya serikali ya Kenya kuvifungia vituo vitatu huru vya television nchini Kenya richa ya maamuzi ya mahakama kuitaka serikali kuondoa marufuku hiyo .
Akizungumza msemaji wa haki za binadamu ,Rupert Colville ,anasema ofisi ya Umoja wa Mataifa inawasiwasi kwa Serikali ya Kenya kukataa kuheshimu maamuzi ya Mahakama Kuu ya Kenya ya kuruhusu vituo hivyo vya Televisheni kuanza tena kurusha matangazo yao.Anaendelea kwa kusema Serikali haina budi kuheshimu na kutekeleza maamuzi ya kisheria .
Rupert Colville ,Ameendelea kwa kusema kuwa tuna wasiwasi pia na majaribio yake ya kuingilia katika haki ya uhuru wa kujieleza kwa kuripotiwa kuonya kwamba ushiriki katika sherehe ya bwana Odinga itapelekewa kufutiwa` Leseni zao. na Taasisi za habari ambazo zimepuuza ushauri huo zimefungiwa shughuli zao.
Na mwandish wetu
George Mwita.
No comments
Post a Comment