Header Ads

Header ADS

Serikali imewataka watendaji wasitumie vitisho na ubabe kwa wananchi















                      Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amewataka watendaji wa serikali kutotumia lugha za vitisho na ubabe kwa wananchi wanaowaongoza.
                       Hayo yametolewa leo mjini dodoma wakati akiahirisha Bunge katika kuhakikisha serikali inatekeleza ahadi zake kwa wananchi.Majaliwa amewataka watendaji wa kada zote serikalini  wasitumie ubabe na vitisho katika utendaji wa kazi zao ili watoe huduma bora kwa wananchi na hatimaye kumaliza kabisa kero za wananchi.
                  Waziri  Mkuu Kassimu Majaliwa ,amesema Serikali imepanga kusambaza umeme wa gridi katika vijiji zaidi ya 7000 na vijiji 7500 kusambaziwa umeme usio wa gridi katika mpango wa REA ,ambapo utawasaidia wananchi kwa kiasi kikubwa kwa sababu umeme ni hitaji ya wananchi.

                  Pia ,amesema kuwa agizo la Rais Magufuli la kujenga ukuta katika mgodi wa  mererani ,ujenzi wa ukuta huo wenye urefu wa zaidi ya kilometa 20 upo katika hatua za mwisho za kukamilika. Majaliwa amesema kuwa Serikali imepeleka moja kwa moja bilion 124  katika kugharamia elimu bure katika shule za misingi na Sekondari  nchini na kuwashauri wazazi na walezi kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kwa kuwapeleka watoto shuleni wapate elimu iliyokusudiwa kutolewa na serikali.

                Suala la michango shuleni ,Waziri mkuu amesema  inaruhusiwa kwa mtu mmoja mmoja ,kikundi cha watu au taasisi kwa ujumla na kupelekwa kwa Mkurugenzi ili ashirikishe bodi ya shule na walimu wasisumbuliwe na baadala yake kuwaacha wajikite katika ufundishaji tu.

No comments

Powered by Blogger.