Watanzania wanataka katiba mpye yenye kuruhusu kupinga matokeo ya urais mahakamani
Prof : Mwesiga Baregu ,asisitiza kuwa kuna umhimu wa kuwepo kwa katiba mpya ili tunapoingia kwenye chaguzi zote mbili isilete shida ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Ni mhimu kuwepo kwa katiba mpya ili nchi isiingie kwenye machafuko.
Mwesiga Baregu ,ambaye ni Muadhiri wa muda mrefu wa Chuo Kikuu cha Daresalam na ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ,amesema bila kupata katiba mpya basi katika uchaguzi wa mwaka 2020 Taifa linaweza kuingia katika machafuko .
Pia ameendelea kusema kuwa dalili zipo wazi za Nchi kuingia katika migongano "Tumeshuhudia uchaguzi wa mdogo wa juzi jinsi mambo yalivyotokea tusitake nchi ifike huko sasa ni wajibu wa kuwa na katiba mpya kuelekea kwenye uchaguzi 2020 ili nchi ivuke salama " Alisema Mwesiga.
Aidha ,ametoa mapendekezo kuwa miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuwa na Tume huru ya uchaguzi ilikuwa na matokeo yenye kusadikika na ya kweli na siyo Tume tulizonazo sasa ambazo zinapanga matokeo na kuamua nani ashinde.
Kwa mjibu wa Baregu ,amesema jambo lingine ni kufanyiwa marekebisho kuwa na mgombea huru katika chaguzi ili endapo mtu atahitaji kugombea haina haja kuwa na chama ndipo apewe nafasi ya kugombea katika nafasi ya uchaguzi .
No comments
Post a Comment