Rais Jonh Magufuli azindua barabara ya Isaka Ushiromba
Rais Jonh Pombe Magufuli ,ahutubia wananchi wa Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa barabara ya Isaka -Ushirombo yenye urefu wa kilometa 132 .
Ni wananchi wa Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga wakisikiliza hutuba ya Rais Magufuli wakati wa kuzindua barabara yenye kilometa 132.Katika uzinduzi wa barabara hiyo Rais , ametumia fursa hiyo na kusema kuwa barabara hiyo ni chachu ya ukuaji wa uchumi na kiungo cha Mikoa ,Shinyanga ,Geita na Kagera pia ni sehemu ya kurahisisha na kuimalisha mahusiano chanya ya kibiashara baina ya Nchi za Uganda ,Rwanda na Burundi .
Pia amewataka wafanya biashara kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya Dawa kwani Serikali inatumia zaidi ya shiling bilion 269 kununua dawa nje ya nchi hivyo endapo wafanyabiashara watajenga viwanda hivyo Serikali itawanufaisha wafanyabiashara wa ndani.
Imetumwa na mwandishi wetu GEORGE MWITA .
No comments
Post a Comment