Serikali nchini Burundi yakanusha takwimu za wakimbizi za UNHCR
Serikali ya Burundi imekanusha takwimu za Umoja wa Kimataifa unaowahudumia wakimbizi UNHCR ,Kuwa wakimbizi wa Kirundi zaidi 430,000 wanahitaji misaada mwaka huu.
Hayo yametokea wakati shirika hilo limeanza kampeni ya kuchangisha pesa zaidi ya dola milioni mia tatu [300] kwa ajili ya kuwa hudumia wakimbizi ambao asilimia 80 wanaishi katika kambi za wakimbizi kwenye mataifa jirani .
Kwa mjibu wa Serikali ya Burundi inasemakuwa UNHCR ,Imekuwa ikidanganya juu ya idadi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi ili wajipatie kiwango kikubwa cha misaada kutoka kwa wafadhili.
No comments
Post a Comment