Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa wanne kwa kugushi Nyaraka za Serikali,
Watuhumiwa wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro kwa kukutwa na Nyaraka za Bandia 240 za Serikali ambazo walikuwa wakizitengeneza kwa njia za udanganyifu pa moja na mihuri 159 na kuuza kwa shilingi elfu ishirini .
Watuhumiwa hao ni Athumani Selemani mwenye umuri wa miaka 71,ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa Serikali katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ,Justine Mziray mwenye umuri wa miaka 55 ,huyu ni mtaalamu wa kuchonga mihuri ,Sporah Daudi ,ambaye ni muandaaji wa nyaraka hizo na kuchapa maandishi kwa kutumia mashine maalumu ,pa moja na Costa Lyatuu , ambaye ni mtaalamu wa kugushi sahihi
Kwa mjibu wa Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro watuhumiwa wamekamatwa wakiwa na nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vyeti vya Kuzaliwa ,Vyeti vya Ubatizo ,Vyeti vya Ndoa ,Vyeti vya Kliniki na matamko ya vizazi na vifo pa moja na mihuri mbalimbali ambayo ni ile inayotumika wakati wa usajli wa Vifo katika Manispaa ya Moshi na Kiteto Mkoani Tabora.
Kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro ,Kamisheni Msaidizi wa Polisi Hamiss Issa amesema kuwa vifaa vingine vilivyo kamatwa ni pamoja na Mashine moja ya kuandikia na kifaa cha kuwekea namba .

No comments
Post a Comment