Header Ads

Header ADS

Waandishi wa Habari wakamatwa na Wanajeshi Nchini Uganda

   Kulingana na maandamano yaliyotokea sehemu mbalimbali nchini Uganda Wanajeshi wamewakamata na kuwatia nguvuni Waandishi wa habari akiwemo mpiga picha wa shirika la habari la  Reuters  James Akena .














              Ikiwa  maandamano hayo nisehemu ya  shinikizo la wafuasi  wa Mbunge  Robert Kyagulanyi  maarufu kwa jina la Bobi Wine  wakitaka aachiliwe huru  na waandamanaji kadhaa wamejikuta wakikamatwa na wanajeshi.
             Kwa upande wa wafuasi wa Bobi Wine walisikika wakiimba   "Nguvu za watu , nguvu zetu"huku wakiwasha moto katikati ya barabara  na kuzuia magari yasipite pamoja na kusimamisha shughuli za kibiashara katika Soko la Kiseka, Barabara za namirembe na Kikubo  kabla ya kusambaa katika mitaa ya  Wandegeya , Makindya pa moja na Gayaza  yenye shughuli nyingi zaidi jijini Kampala.
           Kwa mjibu wa maandamano ya Juma pili kifo cha mtu mmoja kinaripotiwa kutokea wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya waandamanaji  Mjini Miyana  baada ya kupigwa na risasi .
          Rais Yoweri Mseveni amedai kwamba Mbunge Bobi Wine  na Wenzake walikuwa wamelenga kumuua kwa kumpiga mawe pia amevishutumu vyombo vya habari  kwa kile alichokitaja kuwa ni kueneza habari za uongo kwamba wanasiasa wa upinzani walipigwa na kuumizwa  vibaya mikononi wa maofisa wa Polisi  walipokuwa wakiwakamata.

No comments

Powered by Blogger.