CHADEMA, Jimbo la Makambako Mkoa wa Njombe kimemtumbua Mwenyekiti wa Chama jimbo la Makambako.
Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Makambako Mkoa wa Njombe umemfuta uanachama Mwenyekiti wa Chama hicho katika Jimbo la Makambako ambaye ni Diwani wa Kata ya Mjimwema Mheshimiwa Nolascal Mlowe.
Akizungumza na Mtandao huu Katibu wa Chadema Jimbo la Makambako ambaye ni Diwani katika kata ya Makambako Mh. Devid Tweve ,amesemakuwa kamati kuu ya chama imekaa ikajiridhisha na mwenendo wa Mwenyekiti huyo Mh : Mlowe na kubaini kuwa ametoka muda mrefu anakihujumu Chama hicho pamoja na wananchi waliompa kura kupitia Chadema.
Mh : Tweve ameendelea kusema kuwa ameshindwa kuwatetea wananchi kama chama kilivyoaidi wakati wa kumnadi kwenye kampeni na kuruhusu kutumia nguvu kwa kutumia migambo hasa wakati wa ukusanyaji michango ambayo ni ya hiari kwa wananchi kinyumbe na matakwa ya Chama. Pia amesema kamati tendaji ilikaa na kumhoji na yeye hakuwa na majibu ya kusema ndipo kamati tendaji ilikubaliana kumnyang'anya kadi na kumvua uanachama kuanzia jana juma nne tarehe 25 /9/2018 na kutangaza kuwa siyo mwanachama na siyo kiongozi tena wa chama na hata Serikali kupitia chama hicho.
Kwa upande wake Mh: Nolasco Mlowe ,amekili kujivua uanachama pamoja na nafasi zote alizokuwa nazo ndani ya Chama pamoja na kuachia ngazi ya udiwani na kuandika barua ya kuachia nafasi hiyo ya Udiwani kata ya Mjimwema na kupeleka kwa Mkurugenzi wa Halmashuri ya Mji Makambako.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo amekili kupokea barua kutoka kwa bwana Mlowe na kutangaza kuwa Kata ya Mjimwema katika Jimbo la Makambako ipowazi.Pia Mlowa amesema kuwa atakuwa tayari kuenda chama cha Mapinduzi endapo watampokea kwani kuhama chama ni haki ya Kidemokrasia.
Alipo ulizwa kuhusu kurudi tena kugombea Udiwani amesema kuwa atakuwatayari kugombea kwani ni haki ya kikatiba kwani sababu iliyomfanya kuondoka Chadema ni kutokana na migogoro iliyopo ndani ya Chama hicho.

No comments
Post a Comment