Header Ads

Header ADS

LHRC : Yafikisha miaka23 tangu kuanzishwa

                  Kituo cha Sheria na haki za binadamu leo Septemba 26, 2018 kimefikisha miaka 23 tangu kuanzishwa kwake .Huku kikitaja mafanikio kuwa ni kuwajengea Watanzania  juu ya Sheria na haki za binadamu.















           Hayo yamesemwa na Mkurugenzi  wa shirika hilo  LHRC ,Anna Henga  katika kuazimisha miaka 23ya utendaji kazi wa kituo hicho .Pia kumekuwepo uelewa mkubwa  wa haki na sheria hapa nchini Tanzania
          Anna , amesema kuwa kituo hicho kimekuwa chachu ya mabadiliko ya sera  na kutungwa kwa sheria mbalimbali  ikiwemo sheria ya msaada wa kisheria  ya mwaka 2017 na kuendelea kusema kuwa LHRC ,Imeibua mambo mbalimbali yaliyo pelekea uwajibikaji katika ulinzi rasilimali za nchi.
        Hata hivyo Henga amesema kuwa kituo kimekuwa na changamoto kubwa ikiwa nipamoja na kuhusishwa na  shughuli za kisiasa
     " Sisi si wanasiasa  ila tunaweza kumtetea mwanasiasa endapo haki zake zitakiukwa  hivyo si sahihi kutuhusisha na shughuli za kisiasa " Alisema , Henga.
    "Hivyo hupelekea wananchi kuamini propaganda  zenye lengo la kudhoofisha  juhudi za kituo  za kufikia Tanzania inayoheshimu misingi ya haki za binadamu na utawala bora "

No comments

Powered by Blogger.