Jafo awakalia koo wahandisi .
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa [TAMISEMI] Selemani Jafo amewataka wahandisi washauri wanaosimamia miradi ya barabara mbailimbali hapa nchini kuwa upande wa serikali ili kuthibiti ubora wa barabara zinazoendelea kujengwa hapa nchini .
Hayo ameyasema wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara zinazojengwa katika jiji la Arusha kupitia mradi wa mpango mji mkakati [[TSCP],Tanzania Strategic Cities Projects, Unaosimamiwa na ofisi ya Rais TAMISEMI.
Jafo ameongeza kwa kusema kuwa Mhandisi mshauri anapaswa kisimama na serikali na kutoa ushauri wenye tija na utakao leta matokeo chanya katika utekelezaji wa miradi badala ya kuwatetea wamiliki wa kampuni zinazojenga miundombinu hiyo.
Kwa mjibu wa Waziri huyo amesema kuwa Serikali imetoa hela nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye maendeleo hususani miundo mbinu ya barabara ni vyema sasa wataalamu washauri mkawa bega kwa bega na Serikali ili kuepusha hasara inayoweza kujitokeza huko mbeleni endapo miradi hii isipojengwa kwa kiwango.
Pia amesema kuwa hajaridhishwa na hali ya uchafuzi wa mazingira kwenye mitaro mbalimbali ya Jiji na Arusha na kuagiza kwa wahusika mitaro hiyo kufanyiwa usafi mara kwa mara ili kuhakikisha jiji linakuwa safi na barabara zinazoendelea kujengwa zinadumu kwa muda mrefu .
No comments
Post a Comment