Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Makambako Mkoa wa Njombe kimefanya ufunguzi wa uchangiaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Jimbo la Makambako
Agenda kuu ya Mkutano ikiwa ni kutangaza uchaguzi wa ndani ya chama kuanzia matawi hadi Kata ambao unategemea kuanza kesho Juma pili tarehe 16 septemba 2018 katika Jimbo la Makambako.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Jimbo la Makambako Mheshimiwa Onolasco Mlowe amesema kuwa uchaguzi utaanza kwa ngazi ya matawi na baadaye hadi kata na utaratibu utakuwa ni kujaza fomu kwa kila mgombea.
Pia chama hicho kimesema kila jumamosi na juma pili kitakuwa` kinafanya uchaguzi katika matawi yaliyopo ndani ya Jimbo la Makambako.
Pia chama hicho kiliambatanisha na agenda ya uzinduzi wa halambee ya kuchangia mchango kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya Jimbo la Makambako ambapo fedha tasilimu zimechangwa na kufikia kiasi sh milioni moja na lakimbili ikiwa ni Mpango mkakati wa chama hicho wa mwaka 2018 /2019.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi ngazi ya Mkoa wa njombe umemtambulisha pia Mwenyekiti mpya wa Mkoa wa Njombe Mh .Siwale ambaye kitaaluma pia ni mwanasheria wa kujitegemea .Mabadiliko hayo ya mwenyekiti wa Mkoa yamefanyika ikiwa baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa huo kuhama chama na kuhamia CCM kwa madai kuwa anaunga mkono juhudi za Raisi.
Ikumbukwe kuwa kwa kipindi hiki cha awamu ya tano watanzania tumeshuhudia viongozi wengi wakihama vyama vyao na kuhamia CCM ,ambacho ndio chama tawala na ikiwa wote wanatoa sababu moja tu ya kumuunga mkono Raisi, wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mwenyekiyi wa Jimbo amisisitiza kwa vionozi wa Kata na Matawi kuhakikisha wana toa ushirikiano kuhakikisha swala la uchaguzi linakamelika na kuhakikisha viongozi wa matawi husika na kata husika kuhakikisha wanaandaa mazingira ya kufanyia uchaguzi.
Nae Mwenyekiti Mpya wa Mkoa wa Njombe bwana Siwale amewashukuru wanachama kwa mwitikio wa kuweza kufika katika Mkutano huo pia amewataka wagombea wote wa nafasi mbalimbali ndani ya chama kukubaliana na matokeo na kutokuweka makundi mbalimbali ndani ya chama kwani wote ni wamoja "Atakaye shindwa akubaliane na matokeo na ajipange siku nyingine " alisema Siwale.
No comments
Post a Comment