Header Ads

Header ADS

Tume ya Taifa Uchaguzi NEC , imepiga marufuku watumishi wa Serikali kusimamia uchaguzi.

















                 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC ] Dk .Athumani Kihamia amesema tayari Tume imeshatuma jopo la watendaji ili kusimamia kazi za uhakiki  na kusimamia shughuli zote zinazotakiwa  kuendeshwa na Tume ili kuondoa dosari zinazojitokeza wakati wa Uchaguzi.
                Pia amesema kuwa Tume imewapa vitazamio waangalizi hao wa Uchaguzi ili kuhakikisha kila kinachofanyika kabla na baada ya uchaguzi.Amesema kuwa kwa kipindi hiki hakuna mtendaji wa Serikali atakaye simamia bali atakuwa ni Afisa wa Tume ambaye amekula kiapo cha kuacha kazi zake zote za kichama na kila kitu kinakuwa pembeni  na anakuwa chini ya Sheria za Tume " Amesema Dk .Kihamia ".
               Aidha amesema kuwa waangalizi wa Uchaguzi wanakuwa  chini ya Tume kwa siku 60 kwa mjibu wa sheria kwa hiyo katika kipindi chote cha kampeni  hadi kukamilisha upigaji wa kura hadi kutangza mshindi ndipo anaporejea katika majukumu yake ya kawaida na si kweli kwamba Tume hutumia Viongozi wa Serikali bali ni Wananchi kukosa uelewa juu ya hilo.
              Ikumbukwe kuwa Uchaguzi mdogo wa marudio unaotakiwa kufanyika Septemba mwaka huu katika Jimbo la Ukonga umekuwa na mvuto baina ya chama cha CCM na chama cha Chadema  kutokana na Wagombea wake kuonekana ndio wenye  upinzani mkubwa mara baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chadema Mwita Waitara kujiuzulu kwa lengo la kumuunga Mkono juhudi za mheshimiwa Rais na kurejea kugombea tena kwa tiketi ya CCM.

No comments

Powered by Blogger.