Header Ads

Header ADS

Mseveni atoa onyo kwa nchi za magharibi

      Rais wa Uganda Yoweri  Mseveni  ,amezitaka nchi za Magharibi kutoingilia siasa  za nchi hiyo kwani ni mambo ya ndani.Pia amezituhumu nchi za Magharibi ambazo hakuzitaja majina kuwa zinafanya siasa za kuingilia nchi hiyo ya Uganda kwa kutoa misaada kwa Vyama vya Upinzani  kupitia mgongo wa mashirika yasiyo ya kiserlikali .[NGOs].














          Mseveni amesemakuwa ni muhimu kwa Mataifa ya nje kukaa mbali na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine " Alisema kwenye mkutano wake na  vyombo vya habari.na kuendelea kusema kuwa kama kuna tatizo lolote ndani ya Uganda ninauhakika nitalishughulikia vizuri zaidi  ya watu wa mataifa mengine .NGOs, ambazo zinafadhiriwa na nchi za kigeni kwaajili ya kutoa fedha kwa wanasiasa wa upinzani  zinatoa ushauri na uongo kwa nia mbaya.
        Mseveni ameendelea kusema kuwa Serikali yake imeongeza  zaidi ya walinzi 1000 katika jiji la Kampala kwa lengo la kuimarisha ulinzi kufuatia matukio ya watu mashuhuri ikiwa ni pamoja  na maafisa wawili wa Polisi  Mbunge  na mwendesha mashitaka .
       Mseveni ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu Mwanasheria Robert Bobi wine  Kyagulanyi ambaye ni Mbunge na ni Mwanamziki  maarufu kuitaka  Marekani kusitisha misaada ya Kijeshi  kwa Uganda akidai kuwa misaada hiyo inatumika kuwa tesa wananchi .
      Ikumbukwe kuwa  Mbunge huyo maarufu na msanii Bobi Wine yuko Marekani kwa matibabu kutokana na kipigo alichopewa na Askari wa kikosi cha Jeshi kwa tuhuma za kusababisha  vurugu na wafuasi wake kushambulia gari la msafara  wa Rais .
       Bobi Wine alikutana na Mbunge wa Marekani katika juhudi za kutaka Serikali ya Donald Trump ,Isiendelee kuisaidia Uganda  Silaha za Kijeshi.

No comments

Powered by Blogger.