''Haki lazima itendeke hapa''.Asema Bernard Membe
Bernard Membe ambaye aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje wa awamu ya nne,ameingilia kati kuhusu kesi ya mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera kuitaji aachiwe huru bila masharti yoyote.
Kiongozi huyo ambaye anakuwa ni wa pili wa ngazi za juu kungana na baadhi ya Watanzania ambao wanaotaka Kabendera aachiwe huru baada ya kauli hiyo kutolewa pia na Mbunge wa Kigoma mjini,ACT-Wazalendo,Zitto Kabwe na kuanzisha kwa kampeni mitandaoni ya kutaka mwandishi huyo aachiwe huru.
Membe amesema kuwa anaungana na mamia ya Wananchi wanaliounga mkono kampeni ya Zitto ya kutaka kuwa Kabendera aachiwe huru pasipokuwa na masharti yeyote.
Pia,Membe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ameandika kuwa anaungana na mama mzazi wa Kabendera kupaza sauti kuomba serikali imuachie Kabendera huru bila masharti yeyote.
Aidha,Membe amesema kuwa Tanzania ni Nchi kubwa na ina sifa kubwa ya kutenda haki na uhuru wa kukumbatia uhuru waandishi wa habari.
''Niungane na mama mzazi wa Erick Kabendera na Watanzania wengine kupaza sauti yangu kuomba serikali imuachie Erick Kabendera bila masharti yoyote,Tanzania ina sifa moja kubwa nayo ni kutenda haki''.Membe ameandika katika ukurasa wake wa kijamii.
Hata hivyo,ni mara chache sana kwa kiongozi aliyewahi kushika nafasi ya juu serikalini kutoa msimamo na mawazo yake hadharani na kutaka haki itendeke.

No comments
Post a Comment