Wakuu wa Mikoa kucharukiwa na Dkt Bashiru Ally,'Mjitafakari'
Dtk, Bashiru Ally ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi[CCM],amewapa onyo Wakuu wa Mikoa ya Morogoro,Dtk Steven Kebwe na Mkuu wa MKoa wa Mwanza John Mongella.Kutokana na shughuli za Serikali katika maeneo yao kutosimamiwa vizuri.
Onyo hilo limetolewa jana katika Maadhimisho ya kilele cha Wakulima[Nanenane] yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi,Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wakati akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi[CCM].
Pia ameeleza kuwa Dkt Kebwe ameshindwa kumshughulikia Mkurugenzi wa Halmashauri iliyo chini yake anayedaiwa kutumia Sh.Millioni 60 zilozotolewa kwaajili ya Matumizi maalum ya kununua dawa za mchwa.
Kitendo hicho kilichomshinda Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe mpaka pale Rais Magufuli alipoamua kumtumbua mtu huyo.Dkt Bashiru ameeleza kwamba hiyo ni tafsiri kuwa mtu huyo ameshindwa kusimamia majukumu yake.
Hali kadhalika RC Mongella ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,ameonywa na Dkt Bashiru kuhusu kumsimamia na kumbana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema aliyeshindwa kutaja kiwango cha bajeti ya Miundombinu ya Barabara.
''Nisitoke hapa bila kumlaumu mmoja wapo katika timu iliyopo Serikalini kwa nia njema kabisa ili mwaka kesho naye ajirekebishe nadhani Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ujumbe wangu mmeupata,hayo yote ni kwaajili ya kujenga,timiza majukumu yenu''.Amesema Dkt Bashiru.
Vilevile,Dkt Bashiru amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Magufuli pamoja na Mawaziri wake kwa kusimamia utekelezaji wa Miradi ya chama hicho tawala katika Maeneo ya Simiyu na Mwanza.

No comments
Post a Comment