'Haki za raia kisheria'Tanzania Marekani,Uingereza zatilia shaka
Ubalozi wa Uingereza na Marekani wametoa tamko la pamoja kuhusu kile walichokiita''Wasiwasi wa kuzorota kwa haki za kisheria Nchini Tanzania''.
Ofisi hizo mbili za Ubalozi katika tamko hilo wadai kuwa imedhihirika watu kutiwa kizuizini kwa muda Nchini Tanzania bila kuperekwa Mahakamani na kubadilishiwa mashtaka na mamlaka zake za kisheria zaidi ya mara moja.
''Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni--jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa,kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera ,ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na Mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake,ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa jinai''.Inasema sehemu ya tamko hilo.
''Tunaisihi Serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria kwa raia wake,kama ilivotambua kwamba ni haki ya msingi na kuridhia kwenye mikataba mbalimbali ya haki za kibinadam ya Umoja wa Mataifa,miongoni mwao ikiwemo azimio la kimataifa la haki za kiraia na kisiasa''.
Ikiwa ni wiki moja tokea Erick Kabendera apandishwe kizimbani toka alipokamatwa na vyombo vya Usalama Nchini Tanzania.
Ubadhirifu wa kiuchumi,Moshi anashtakiwa kwa kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu uchumi,pili kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya million mia moja sabini za kitanzania na tatu,Utakatishaji wa fedha zenye thamani ya million mia moja na sabini.Hayo ni jumla ya makosa matatu aliyoshtakiwa Mwandishi huyo.
Namna ambavyo alivokamatwa,na taswira inayoonekana na hatua hiyo kwa uhuru wa vyombo vya habari Nchini humo kumekuwa na wasiwasi ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa baadhi ya wanaharakati wameonyesha kushangaza na kubadilika kwa yaliaminika kuwa ndio makosa anayotuhumiwa nayo.
Mwanzo wale wa Idara ya uamiaji na Maafisa Polisi walisema anchumguzwa kuhusu utata wa Uraia wake.
Mawakili wake baadae walitoa taarifa wakieleza mteja wao atashtakiwa kwa kuhusika na ripoti iliyochapishwa katika jarida la The Economist,lakini mahakamani kibao kikageuka tena na kuwa kesi ya ubadhirifu Uchumi.
Ofisi hizo mbili za Ubalozi katika tamko hilo wadai kuwa imedhihirika watu kutiwa kizuizini kwa muda Nchini Tanzania bila kuperekwa Mahakamani na kubadilishiwa mashtaka na mamlaka zake za kisheria zaidi ya mara moja.
''Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni--jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa,kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera ,ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na Mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake,ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa jinai''.Inasema sehemu ya tamko hilo.
''Tunaisihi Serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria kwa raia wake,kama ilivotambua kwamba ni haki ya msingi na kuridhia kwenye mikataba mbalimbali ya haki za kibinadam ya Umoja wa Mataifa,miongoni mwao ikiwemo azimio la kimataifa la haki za kiraia na kisiasa''.
Ikiwa ni wiki moja tokea Erick Kabendera apandishwe kizimbani toka alipokamatwa na vyombo vya Usalama Nchini Tanzania.
Namna ambavyo alivokamatwa,na taswira inayoonekana na hatua hiyo kwa uhuru wa vyombo vya habari Nchini humo kumekuwa na wasiwasi ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa baadhi ya wanaharakati wameonyesha kushangaza na kubadilika kwa yaliaminika kuwa ndio makosa anayotuhumiwa nayo.
Mwanzo wale wa Idara ya uamiaji na Maafisa Polisi walisema anchumguzwa kuhusu utata wa Uraia wake.
Mawakili wake baadae walitoa taarifa wakieleza mteja wao atashtakiwa kwa kuhusika na ripoti iliyochapishwa katika jarida la The Economist,lakini mahakamani kibao kikageuka tena na kuwa kesi ya ubadhirifu Uchumi.
No comments
Post a Comment